MBOWE ALALAMIKA KUNYANG'ANYWA GARI LA SERIKALI

Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe amesema amenyang’anywa gari la serikali alilokuwa akitumia na Ofisi ya Bunge ambalo ni haki yake kuwa nalo.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Jumatano Aprili 4, Mbowe alisema amenyang’anywa gari hilo tangu Januari, mwaka huu.


“Sina gari la serikali wala dereva, nilinyang’anywa tangu Januari natembelea gari binafsi kwa sasa, licha ya kuwa ni haki yangu.


“Lakini mimi sijililii mwenyewe, ninayo magari mengi nitatumia na hata nikikosa wabunge hapa watanipa gari la kutembelea,” alisema Mbowe bila kuelezea zaidi sababu za kunyang’anywa gari hilo.


Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akijibu tuhuma hizo amesema gari lipo isipokuwa Mbowe mwenyewe ndiyo hataki kulitumia.


“Gari la kiongozi wa upinzani lipo na dereva yupo, ila Mbowe halitaki gari wala dereva,” amesema Kagaigai.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527