MAKONDA AWATOLEA UVIVU MAWAZIRI WANAOMPONDA KAMPENI YAKE YA WATOTO KUTELEKEZWA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wale wote wanaosema kampeni yake ya kuwasaidia akina mama waliotelekezwa na watoto imevunja sheria, pengine wana watoto nje na wanaogopa kujitokeza.


Makonda ameyasema hayo leo Aprili 19,2018 katika uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya mama na mtoto iliyopo Chanika iliyojengwa kwa msaada wa Shirika Maendeleo la Kimataida la Korea (Koica).


“Eti wanasema navunja sheria, natakiwa nifanye faragha kama unataka faragha tunza mtoto. Mimi siogopi, nipo tayari kufungwa lakini kwa ajili wa kutetea haki za watoto. Pengine hao wanaosema navunja sheria wana watoto wao nje wanaogopa kujitokeza,” amesema.

Jana, Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi akiwa bungeni alisema kampeni hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika faragha na sio kama inavyofanyika sasa.

Awali, Waziri wa Afya, Jinsia, Wanawake na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha, lakini akasema kwa sasa inafanyika huku picha za watoto zikifichwa.

Aliyeibua hilo bungeni jana alikuwa ni mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyehoji uhalali wa kampeni hiyo na akahoji kama haivunji sheria na kuwavunjia haki wanawake na watoto.

Na Asna Kaniki, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527