ASKOFU MORAVIAN AWATAKA WATANZANIA KUACHA KULALAMIKA

Askofu Kiongozi wa Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi Alinikisa Cheyo, amewaasa Watanzania kuacha kulalamika na badala yake wajikite katika kufanya kazi njema inayompendeza Mungu.


Askofu Cheyo ametoa kauli hiyo katika ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Mbeya Mjini.

Askofu amesema ili Watanzania waweze kujiletea maendeleo yenye tija kufikia uchumi wa kati wanapaswa kuachana na mambo ya kisiasaili waweze kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.

Askofu Cheyo pia ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wake wengine wa dini nchini kutofautisha dini na siasa ili kujenga upendo miongoni mwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha amani ya nchi.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.