ABDUL NONDO ABANWA UHAMIAJI..ANATAKIWA APELEKE VYETI VYA KUZALIWA VYA BABA, MAMA, BABU, BIBI

Mwanasheria TSNP, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria TSNP, Paul Kisabo amesema kuwa ni takribani wiki sasa Mwenyekiti wao wa Mtandao wa Wanafunzi(TSNP), Abdul Nondo amekuwa akihitajika uhamiaji ili akahojiwe uraia wake na pamoja na wazazi wake.


Kisabo ameeleza kuwa jambo hilo la kuhojiwa uraia wake wamelitimiza jana baada ya kutoka Mahakama Kuu kwenye kesi yake iliyohairishwa mpaka tarehe 11, April mwaka huu.


Aidha ameeleza kwamba Kwa muda wa takribani wiki moja mpaka sasa mwenyekiti wa TSNP Abdul Nondo amekuwa akihitajika uhamiaji ili akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake.


Ameeleza kuwa Nondo hakupata nafasi ya kwenda sababu hakuwa sawa kutokana na changamoto alizokumbana nazo siku za hivi karibuni.


"Mnamo sa sita mchana tuliweza kumfikisha Abdul Nondo makao makuu ya ofisi za uhamiaji mkoa (makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani) na wanataka kupata taarifa zake binafsi, za wazazi wake, babu na bibi zake pande zote mbili (upande wa baba na upande wa mama) pamoja na za ndugu zake,kwani Afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumuhoji mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake.


"Wanamashaka na uraia wa Abdul Nondo, hivyo alitakiwa awathibitishie kuwa yeye ni raia wa Tanzania. Nondo amejaza taarifa zile anazozifahamu tu.


"Baada ya kujaza taarifa hizo, ametakiwa kupelea cheti chake cha kuzaliwa pamoja na vyeti vya wazazi wake wote wawili, babu na bibi zake mnamo April 20, 2018. "Amesema Kisabo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527