ZARI : NATAFUTA PESA MPYA, SIHITAJI MWANAUME

Zari ameibuka na jipya tena huku safari hii akisisitiza kuwa wale wanaume wakware wote waliopanga foleni kusubiri penzi la Zari hawana nafasi kwani hana muda wa kuwa na mpenzi kwa sasa.



Zari alitangaza kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, mwezi uliopita lakini tangu hapo Kumekuwa na tetesi nyingi juu ya Zari kupata mwanaume mwingine wa kuchukua nafasi ya Diamond.


Kupitia kurasa yake ya SnapChat Zari ameweka wazi kuwa haitaji mpenzi kwa sasa baada ya marafiki zake kumtumia ujumbe uliosema; “Kama mwanaume wako akienda kutafuta vimada wenye msambwanda mpya inabidi umkumbushe kuwa na wewe msambwanda wako mpya ni kwa ajili ya mwanaume mpya”.


Zari amedai kuwa marafiki zake wanamtumia meme hizo kama vijembe kwa EX wake lakini amejibu kuwa hataki mwanaume mpya kwa sasa:


"Marafiki zangu siwawezi hivi kwanini wamekazana kunionyesha hizi Mambo lakini hazinifai mimi….. Nahitaji kutafuta pesa mpya na sihitaji mwanaume kwa muda huu samahani!!!!”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527