Tuesday, March 20, 2018

POLISI KIGOMA WAKAMATA SILAHA ZA KIVITA,PEMBE ZA NDOVU

  Malunde       Tuesday, March 20, 2018
Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limefanikiwa kukamata silaha mbili AK 47 zenye namba UB38341997 na risasi 17 ndani ya magazine na AK47 1967TY4577 na risasi 24 ndani ya magazine pamoja na pembe za ndovu vipande 9 katika pori la Makerema Wilayani Kasulu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo Maltin Otieno 
alisema  silaha hizo zilikamatwa katika oparesheni iliyoendeshwa na jeshi la polisi katika pori la Makere wilayani Kasulu ya  kuwasaka majambazi.

Alisema Mach 19 majira ya saa tano usiku kwenye pori la Makere katika Kijiji cha makere Wilayani Kasulu watu wawili waliofahamika kwa majina ya Norbert Andrew maarufu kwa jina la Kipua na Bukuru Steven Mhutu mkimbizi kambi ya Nyarugusu waliuawa kwa kushambuliwa na majambazi wenzao wakati wakienda kuwaonyesha polisi silaha walipokuwa wamezificha porini.

Alisema marehemu wote walikamatwa katika tukio moja la kuvunja kibanda na kuiba ambapo mmoja wa majambazi hao aliangusha simu eneo la tukio iliyowezesha polisi kumkamata na baada ya kuhojiwa na polisi aliwataja wenzake.

Polisi walifanikiwa kukamatwa  majambazi wanne na katika mahojiano walikiri kuhusika na matukio ya mauaji, na uvamizi katika nyumba za watu wilayani hapo, baada ya mahojiano hayo mtuhumiwa aliwaongoza polisi mpaka kambi ya Nyarugusu na kufanikisha kukamatwa mtuhumiwa mwingine na  alipopekuliwa alikutwa na silaha walizokuwa wakizitumia kufanyia uhalifu.

Alisema baada ya kukutwa na silaha hizo alieleza kuwa kuna silaha nyingine tano ambazo amezificha porini ambapo askari waliondoka na watuhumiwa hao na baada ya kufika maeneo wanayoficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao na askari walilala chini na watuhumiwa hao kupigwa risasi na majambazi wenzao na kufariki dunia wakati wakikimbizwa hospitali.


Aidha Kamanda Otieno amewaomba wakimbizi wote walio na silaha kambini kuzisalimisha polisi kabla ya mwezi huu kuisha baada ya hapo wataanza msako utakaosihusisha kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kigoma.


Sambamba na tukio hilo jeshi la polisi linamshilikia mtu mmoja Solomoni Ntihazo kwa Kosa la kukutwa na pembe za ndovu vipande tisa ambapo vipande viwili ni vikubwa na vipande saba ni vidogo.

Na Rhoda Ezekiel -Malunde1 blog

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Maltin Otieno akionesha silaha walizokamata - Picha zote na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Maltin Otieno akionesha silaha hizo


Pembe za ndovu zilizokamatwa
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post