HARMORAPA AMTOLEA POVU UCHEBE NA KUDAI AMEOLEWA NA SHILOLE

Rapa wa muziki wa Bongo fleva Harmorapa aliyejipatia umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kwa vituko vyake amerudi tena na safari hii yuko na Shilole pamoja na mumewe Uchebe.


Harmorapa ameibuka na kudai kuwa Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemuoa mumewe Uchebe. Huku akidai kuwa kitendo cha Uchebe kuacha kazi yake ya ufundi gereji na kumtegemea mke wake ni sawa na kuoelewa.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa amerusha dongo hili lililowaelekea Uchebe na Shilole:


"Uchebe mtoto wa kiume umeacha Kupiga spana umekimbilia Kuolewa. Kwa nini badgirlshishi akuosheshe vyombo? Uchebe mtoto wa kiume rudi gereji ukapige spana la sivyo utapigwa sana vibao na shishi na kufulishwa mpaka chup*, sura yenyewe imekukunjika kama yangu utafikiri tumetoroka kwenye zui la manyani/ hiyo ndio faida ya wanaume marioo vibenteni demu wanahudumia masponsa mzigo tunakula sisi kimya kimya na chup* tunachafua sisi wahudumiaji alafu vibenteni kama Uchebe kazi yao kutakatisha chup*”.


Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana mwishoni, kabla hawajaoana Uchebe alikuwa fundi magari gereji lakini baada ya kufunga ndoa amekuwa akionekana kila mahali na Shilole akimsindikiza kwenye shoo zake zote hali iliyozua maneno maneno.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527