DOGO JANJA AFUNGUKA SABABU YA KUPANGIWA RATIBA YA 'KUHONDOMOLA TENDO LA NDOA' NA MKEWE 'UWOYA'

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja ambaye ni mume halali wa muigizaji wa filamu bongo Irene Pancras Uwoya, ameweka wazi sababu za kupangiwa ratiba na mke wake huyo, jambo ambalo lilizua kizaa zaa baada ya kuiweka kwenye mtandao.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema alishtuka baada ya kuona ratiba hiyo imebandikwa ukutani alipoamka, na kueleza sababu zake.

“Nilikuwa nimelala nimeamka nikakutana na ratiba kwenye ukuta, nikaangalia duh!! nikaipost insta. Unajua yule ni mshkaji wangu sana alikuwa ananitania, na yeye ndiye alianza kuipost, na kimvua hiki uniambie ratiba!!? Atadondoka mtu”, amesema Dogo Janja

Wawili hao walifunga ndoa ya kimya kimya jambo ambao wengi hawaamni mpaka leo kuwa ni wanandoa, na pia kutokana na tofauti ambazo wanaonekana wanazo za kiumri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527