ANGALIA PICHA ZILIZOTIKISA DUNIA

Angalia hapa  picha za matukio ambayo kwa namna moja au nyingine zimegusa maisha ya watu na kuacha gumzo kwa jamii.
Mmoja wa waokoaji nchini Syria Abu Kifah akiwa na wenzake, walifanikiwa kumuokoa mtoto mwenye siku 30 tu tangu azaliwe, kwenye vifusi vilivyoanguka kutokana na mashambulizi yaliyokuwa yakiendelea ya vita, katika mji wa Idlib. Baada ya kumuokoa alimkumbatia kifuani kwake kwa hisia huku akitokwa na machozi akiwa anmkimbiza gari la wagonjwa ili apelekwe hospitali, tukio ambalo lilifanikiwa kupatwa vizuri na vyombo vya habari, na kusababisha gumzo dunia nzima juu ya matukio yanayoendelea Syria.

Muokoaji Abu Kifah akitoa machozi baada ya kumuokoa moto mwenye umri wa siku 30 kutoka kwenye kifusi baada ya shambulizi la bomu nchini Syria.

Mnamo mwezi April 2017, ndege ya kivita iliangusha bomu la kemikali kwenye mji wa Idlibi, na kusababisha madhara kwa wakzi wa eneo hilo hukutakriban watu 100 wakiwemo watoto kufariki kwa sumu kali iyotokana na bomu hilo. Mpaka sasa hajajulikana nani anahusika na bomu hilo kati ya serikali ya Syria, Waasi au Russia ambao ni supportes wakubwa wa serikali ya Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Watoto waliouwa kwa bomu la sumu nchini Syria

Karibia Afrika nzima na dunia tunafahamu kilichotokea nchini Rwanda mwaka 1994, juu ya mauaji ya Kimbari, Wahutu na Watutsi walivyokuwa wanauana. Tukio ambalo mpaka leo limeacha alama kwenye maisha ya Wanyarwanda wengi hata nchi jirani za Afrika Mashariki. Picha hii inaonyesha miili ya watu waliokufa ikiwa imelala nje ya kanisa huko Lukara, ikipigwa na mpiga picha Scott Peterson

Masalia ya miili ya watu wa Rwanda ikiwa imelala mbele ya kanisa

Mwaka 2017 haukuwa mzuri kwa jirani zetu Kenya kufuatia machafuko kadhaa yaliyojitokeza, kutokana na uchaguzi wa Agosti 8. Picha hii ilipigwa na Brian Ganga ikimuonyesha askari polisi akitokwa na machozi, baada ya kushuhudia askari mwenzake akimpiga risasi raia, wakiwa kwenye vurugu. Picha hii ilisambaa sana kwenye vyombop vya habari Afrika na kuacha gumzo kubwa.

Askari akilia kwa kutoa machozi baada ya kushuhudia tukio la mtu kuuawa

Mwaka 2012 tasnia ya habari Tanzania ilipigwa pigo kubwa sana baada ya mwandishi mwenzao Daudi Mwangosi wa mkoani Iringa, kuuawa kikatili na polisi. Picha hii ilipigwa na Joseph Senga (marehemu pia) ikionyesha tukio zima jinsi Daudi Mwangosi alivyouawa kwakupigwa bomu na Polisi. Wahusika walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa miaka 15 jela.
Polisi wakiwa wamemzunguka mwandishi Daudi Mwangosi kabla hajauawa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527