ALIYETAJA ORODHA YA WATU 10 HATARI ZAIDI KWA USALAMA WA TAIFA TANZANIA KUBURUZWA MAHAKAMANI

Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi amefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria Cyprian Musiba kwa kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika tarehe 25 Februari, 2018.


Barua hiyo iliyotolewa na Mwanasheria wa Maria Sarungi, Benedict Alex Ishabakaki imeeleza kuwa mteja wake alitajwa na gazeti la Tanzanite toleo Namba 50 lililotoka Februari 26, 2018 kuwa ni moja ya watu hatari kwenye usalama wa taifa.


Kwa upande mwingine, barua hiyo imeitaka Dar24 kufuta habari hiyo na kuomba radhi hadharani kwa kitendo cha kuandika habari hiyo yenye lengo la kumfedhehesha mteja wao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527