AFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI KWENYE MSAFARA WA RAIS MAGUFULI KAHAMA


Mwili wa Deogratius Landani (47) mkazi wa Kahama ukiwa barabarani baada ya kugongwa na gari kwenye msafara wa rais John Pombe Magufuli wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Mkazi wa Kahama aliyejulikana kwa jina la Deogratius Landani (47) amefariki dunia baada ya kugongwa na gari mojawapo miongoni mwa magari yaliyokuwa katika msafara wa Rais John Pombe Magufuli wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 

Tukio hilo limetokea Jumamosi Machi 10,2018 majira ya saa 7:00 mchana katika mtaa wa Shunu kwenye njia kuu ya kutoka Masumbwe kueleke Kahama wakati magari yakiwa kwenye msafara wa rais Magufuli wilayani Kahama. 

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Kasyombe Mwakyusa Chanzo ni mpanda baiskeli huyo Deogratius Landani kuingilia msafara kwa kuingia barabarani ghafla bila kuchukua tahadhali za kutosha. 

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mji Kahama kwa uchunguzi zaidi.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

ANGALIA VIDEO HAPA CHINI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527