NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS ATEMBELEA VITUO VYA AFYA TINDE NA SAMUYE SHINYANGA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege  leo Ijumaa Februari 23,2018 amefanya ziara ya Kushtukiza katika Kituo cha Afya Tinde na Samuye katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kujionea hali ya ujenzi wa majengo unaoendelea kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.


Naibu Waziri huyo ameona hali ya ujenzi wa jengo la upasuaji,wodi ya wazazi,Wodi ya watoto na jengo la kuhifadhia maiti,jengo la maabara na nyumba ya mtumishi katika kituo cha afya Tinde.

Serikali imetenga shilingi milioni 400 na kituo cha afya Samuye shilingi milioni 500 .Fedha hizo zimepokelewa  katika vituo hivyo mwishoni mwa Mwezi Desemba 2017 na ujenzi unatarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka huu.

Kujengwa kwa vituo hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM kuhakikisha huduma za mama na mtoto zinaboreshwa kwa kiwango cha juu.

Ziara hiyo pia imehudhuriwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga (CCM),Azza Hilal Hamad.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akiwa katika kituo cha afya Tinde kuangalia ujenzi wa majengo mbalimbali unaoendelea. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga (CCM),Azza Hilal Hamad - Picha na Said Nassor - Malunde1 blog
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akiwa katika kituo cha afya Tinde akiwa katika kituo cha afya Tinde akiangalia msingi wa jengo la wodi ya wazazi
Ujenzi wa shimo la kuchomea taka ukiendelea katika kituo cha afya Tinde
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akimweleza jambo Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga (CCM),Azza Hilal Hamad katika kituo cha afya Tinde

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akiangalia jengo la Maabara  katika kituo chaTinde
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akiwa katika jengo la Maabara kituo cha afya Samuye
Picha na Said Nassor - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527