MTUMISHI WA TRA MBARONI KWA TUHUMA YA KULAWITI MTOTO

Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Hassan Abuutwalib maarufu Kiringo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, Hassan Nassir Ali amesema wamemkamata jana (Jumatatu) katika maeneo ya uwanja wa ndege Zanzibar alipokuwa akijaribu kuondoka kuelekea Mwanza.

"Mlalamikaje ambaye mwenye miaka 54 jina lake nalihifadhi alikuja kutoa malalamiko kuwa mtoto wake alichukuliwa na Kiringi na kumpeleka katika nyumba iliyokuwa haijamalizwa kujengwa huko Fuoni uwandani ambapo inadaiwa alifanikiwa kumlawiti baada ya kumpa dawa za kupoteza fahamu na kumsababishia maumivu sehemu zake za siri za nyuma", amesema Kamanda Nassir.

Aidha, Kamanda Nassir amesema uchunguzi wa madaktari ulithibitisha kuathirika sehemu za siri za nyuma za mtoto huyo

Kwa upande mwingine, Kamanda Nassir amesema ameunda timu ya uchunguzi iliyojumuisha wakuu wa upelelezi wa wilaya tatu wilaya ya mjini, wilaya ya Magharibi A na B ili wakachunguze ukweli wa tukio zima lilotokea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527