MTOTO AZALIWA AKIWA NA MAJERAHA YA RISASI MWILINIMtoto mmoja amezaliwa na risasi ndani ya mwili wake katika jimbo la Tenesee nchini Marekani.

Mamaake mwenye umri wa miaka 19 alipigwa risasi katika kisa kimoja kilichohusisha magari mawili barabarani karibu na mji wa Memphis , kulingana na vyombo vya habari.

Mwanamke huyo alikuwa na ujauzito wa wiki 36 wakati alipopigwa risasi.

Alipelekewa hospitalini ambapo alihitaji kufanyiwa upasuaji na ndipo akajifungua mwanae.

Mtoto huyo alizaliwa na majeraha akiwa katika hali mahututi, kulingana na maafisa wa polisi wa Memphis.

Mwanaume aliyeandamana na mwanamke huyo hospitalini aliambia maafisa wa polisi kwamba watu watatu waliokuwa katika gari jeusi aina ya Chevrolet walikaribia gari lao barabarani kabla ya kuwafyatulia risasi kulingana na chombo cha habari cha Fox 2 News.

Mama huyo alipigwa risasi mara tatu katika nyonga yake ya kulia, kituo hicho kiliripoti.


Theme images by rion819. Powered by Blogger.