Friday, February 23, 2018

KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI TIDO MHANDO YAPIGWA KALENDA

  Malunde       Friday, February 23, 2018
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya kusababisha hasara ya Shilingi Milioni 887 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando hadi Februari 28,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).


Mwendesha Mashtaka wa (TAKUKURU), Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kumsomea Tido maelezo ya awali.


Hata hivyo, Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta ameieleza Mahakama kuwa amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya (Ph), hivyo anaomba ahirisho.


Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 28,2018 kwa ajili ya Tido kusomewa (Ph).


Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Tido anakabiliwa na makosa matano ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.


Inadaiwa alilitenda kosa hilo June 16,2008 akiwa Dubai kama mtumishi wa TBC alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mikataba ya uendeshaji wa vipindi kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BVI) bila kutangaza zabuni na kuisababishia channel hiyo kunufaika.


Inadaiwa kati ya June 16 na November 16,2008 akiwa Falme za Kiarabu, kama muajiriwa wa TBC kwa cheo cha Mkurugenzi Mkuu kwa mamlaka yake alilisababishia shirika la TBC hasara ya Sh.Mil 887.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post