JPM ATEUA MWANASHERIA MKUU MPYA WA SERIKALI NA NAIBU WAKE


 
Rais Magufuli amefanya uteuzi mpya kwa kumteua Dk Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli pia amewateua aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu, kuanzia Februari 1,2018.

Kabla ya uteuzi, Dk Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St.Augustine University) kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta, (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority- PURA).
Theme images by rion819. Powered by Blogger.