CCM YAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI UDIWANI ISAMILO...ASILIMIA 2.2 TU NDIYO WALIOPIGA KURA
Mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa kata ya Isamilo jijini Mwanza, Nyamasiriri Marwa ameibuka kidedea kwenye uchaguzi ulioshuhudia asilimia 2.2 pekee ya wapiga kura 18,029 waliandikishwa ndiyo waliojitokeza kupiga kura.


Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Februari 17, Nyamasiriri ametangazwa mshindi kwa kupata kura 2,220 sawa na asilimia 57 ya kura halali 3,920 zilizopigwa.


Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Kiomoni Kibamba mgombea kupitia Chadema, John Kisieri amepata kura 1,678 huku Hashim Omar wa CUF akiambulia kura 22.


Pia, Kabamba amabye ni mkurugenzi wa Jiji la Mwanza amesema wapiga 3,960 walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo.


Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wapiga kura 18,029 waliandikishwa kwenye kata hiyo.


Uchaguzi mdogo kata ya Isamilo umefanyika baada ya Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 yaliyompa ushindi David Chibalwa wa Chadema.

Na Saddam Sadick, Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.