Monday, January 22, 2018

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUTUMIA MAFUNZO YA SIDO KIKAMILIFU

  Malunde       Monday, January 22, 2018

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana akiongea na wajasiriamali mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akifunga mafunzo yaliyokuwa yameandaliwa na SIDO jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuzipa thamani bidhaa wanazozitengeza. Pembeni yake ni Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna -KAJUNASON/MMG.
Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga akitolea ufafanuzi mafunzo hayo ambayo wamekuwa wakiyatoa kwa wajasiriamali mbali mbali ili kuwajengea uwezo wa kuzipa thamani bidhaa zao wanazozitengeneza.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana (wa nne kutoka kushoto) na Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga anayemfuatia wakifurahia jambo na wajasiriamali mara baada ya kuhudhuria sherehe ya kufunga kwa mafunzo yao.
Wajasiriamali wakifurahia bidhaa walizozitenegeza wakati wa mafunzo.


Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana akipata maelekezo ya bidhaa walizozitenegeza wakati wa mafunzo. 

Wajasiriamali wakipokea vyeti.


Wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja.
 ***
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana amewataka wajasiliamali mkoa huo kuhakikisha kuwa wanayatumia vyema mafunzo waliyopata kutoka Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO).

Lyana amesema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa anafunga mafunzo ya siku tano kwa wajasiriamali yanayoendeshwa na Sido kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali wadogo kuweza kusindika na kuongeza thamani bidhaa mbalimbali.

“Sisi kama jiji tumeandaa mpango kabambe wa utalii wa mkoa wa Dar es Salaam amabo utaweza kuwasaidia wajasiriamali wa ndani kuuza bidhaa zao hivyo kila mjasiliamali ahakikishe anajianda kwa kuandaa vitu vyaka katika ubora unaohitajika”, amesema Lyana.

Aidha mkurugenzi huyo aliweka wazi kuwa kama wajasiriamali wote hao wataweza kufanya kama walivyofundishwa wataweza kumsaidia Rais juu ya kuipelekea nchini yetu katika uchumi wa kati ambao unategemea sana Viwanda hivyo kwa wao kila mmoja kama ataanzisha kiwanda kidogo kutaweza kupunguza tatizo la ajira katika baadahi ya maeneo.

Alitoa wito kwa wadau na watu wengine kwenda kujifunza Sido hili iwe rahisi kurasimisha biashara zao ambazo walikuwa wanafanya kienyeji.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post