RAIS MAGUFULI AMMWAGIA NOTI WASTARA..MWENYEWE AFURAHIA MBELE YA SHILAWADU

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwasilisha mchango wa shilingi milioni 15 kwa mwigizaji Wastara kutoka kwa Rais Dkt Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu. SHILAWADU ndio waliomuibua mwigizaji huyo kiasi hata ugonjwa wake uliwagusa wengi pamoja na Rais Magufuli na mkewe.
Samike (wa pili kulia) akiwa na watangazaji wa kipindi cha SHILAWADU baada ya kumkabidhi Wastara fedha hiyo.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na mwigizaji Wastara pamoja na SHILAWADU baada ya kumkabidhi msaada wa 15m/- kutoka kwa Rais Dkt Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu. Pia aliwasilisha mchango wa sh milioni moja na laki tisa toka kwa wasaidizi wa Rais. SHILAWADU ndio waliomuibua mwigizaji huyo kiasi hata ugonjwa wake uliwagusa wengi pamoja na Rais Magufuli na mkewe.


Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amefunguka na kudai hakutegemea kama Rais Magufuli angeweza kulipa kipaumbele tatizo lake alilokuwa kwa sasa huku akimshukuru kwa kuweza kumsaidia suala hilo.

Wastara ameeleza hayo wakati alipokuwa akipokea pesa ya matibabu iliyotolewa na Rais Magufuli na mke wake Mama Janeth jumla ya milioni 15 ili iweze kumsaidia katika matibabu yake kama waliyovyoongea katika simu hapo awali.

"Kubwa niseme tu nashukuru, kwa sababu sikutegemea kama tatizo langu Mhe. Rais angeweza kulipa kipaumbele. Nashukuru pia naomba mpeleke salamu zangu kwa Mhe kwamba natamani siku moja nisimame ili niweze kuwa naye bega kwa bega katika kazi za kujenga nchi yetu ya Tanzania",alisema Wastara.

Pamoja na hayo Wastara ameendelea kwa kusema "natambua kuna watu wengi wana shida, mimi kama mimi natamani nifanye kazi yangu ili niweze kutoa 'percent' yangu niweze kuwasaidia na nimekuwa nikiomba sana muda mwingi jambo hilo".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527