Sunday, December 24, 2017

WENGINE WATATU WA TATUMZUKA WAIBUKA NA VITITA VYA MILIONI 10 KUELEKEA FUNGA MWAKA

  tz       Sunday, December 24, 2017
 .Washindi watatu wa mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka waliojishindia kitita cha Milioni 10 kwa kila mmoja, katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka,wakia katika nyuso za furaha kabisa.
Afisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) ,mapema jana jijini Dar,kuhusiana na washindi watatu wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka waliojishindia kitita cha Milioni 10 kwa kila mmoja, katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka

Afisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious akimkabidhi hundi ya milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka, Anna Nkya kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani), uliofanyika jana jijini Dar es salaam.

***

Wasimamizi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka wametoa washindi watatu wa sh. Milioni 10 katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka ili kuwapa wachezaji wa droo hiyo kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar,wakati wa kukabidhi hundi hizo kwa washindi hao, Mmoja wa Maafisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious amesema droo hiyo inachezwa majira ya saa tatu na nusu usiku ambayo inakwenda hadi mwishoni wa mwaka.

Dina aliwataja washindi hao watatu kuwa ni Hilda Mwaibako,Asha Hamisi pamoja na Anna Ankya,ambao wanatoka katika vitongoji tofauti lakini wote ni wakazi wa jiji la Dar Ess Salaam.

Dina amesema kuwa washindi wote waliopewa hundi ni kutokana na kushinda mchezo huo kwa kufuata taratibu zilizowekwa za mchezo,Amesema Watanzania waendelee kuchangamkia fursa ya mchezo huo na kuibuka washindi na kufurahi msimu wa sikukuuu na ziku zinazoendelea.''Droo ya walioshinda ni maalumu na wakiona umuhimu wataweza kuitumia na droo zingine zikiendelea,''alisema Dina.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post