WAZIRI ATOA SIKU 10 JENGO LA TANESCO LIBOMOLEWE

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku kumi kwa jengo la Tanesco lililopo Ubungo libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara ya Morogoro.


Waziri huyo pia amewataka watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo na wakandarasi waliowekwa kubomoa jengo hilo wasisafiri wala kusherekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali washughulikie jengo hilo kuvunjwa.


“Nataka kuanzia leo Desemba 22 ndani ya siku sita jengo hili lote libomoke na kwasababu ni majengo mawili ndani ya siku kumi majengo yote mawili yawe yamebomoka kama mnaona vigumu kubomoa jengo lenu waambieni TBL ”amesema


Amesema hadi kufikia mwisho wa mwezi huu jengo hilo lote liwe limeanguka chini na hakuna cha sikukuu wala Krisimasi kwenye kubomoa jengo hili na ujenzi wa barabara kama Tanesco wanaaza waanze tusiwakwamishe”amesema.


Amesema wananchi wameshabomoa majengo yao kwanini Tanesco bado wanasuasua na kudai Januari mosi ataenda tena kukagua kuona kama agizo lake limefanyiwa kazi.


“Naimani wananchi hawatapata shida wakati wa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya ,kwa hiyo asiruhusiwe mtumishi yoyote wa Tanesco kwenda nje ya ofisi yake wakati wa sikukuu zote mbili”amesema


Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Kahitwa Bishaija amesema wamelisikia agizo la Waziri na wataenda kulitekeleza kama lilivyo.

Na Jackline Masinde,Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527