Tuesday, December 26, 2017

WANASAYANSI WAPATA NGURUWE WENYE SURA MBAYA ZAIDI DUNIANI

  Malunde       Tuesday, December 26, 2017

Wanasayansi wamepata picha za kwanza za msituni za kati ya nguruwe wachache wenye sura mbaya zaidi duniani.

Nguruwe hao kwa jina Javan waty, wako kwenye hatari ya kuwindwa na kupotea kwa makaazi yao, na wanasayansi wanasema kuwa nguruwe hao tayari wanaelekea kuangamia.
Kamera fiche kwa sasa zimefichua kuwa idadi ndogo wa nguruwe hao bado wanaishi maeneo ya misitu kadha huko Java.

Wanasayansi wanasema kuwa lengo lao ni kulinda makazi ya wanyama hao.Kamera fiche kwa sasa zimefichua kuwa idadi ndogo wa nguruwe hao bado wanaishi maeneo ya misitu kadha huko Java.

Mkuu wa utafiti huo Dr Johanna Rode-Margono, alisema kuwa wanasayansi walifurahishwa kugundua kuwa nguruwe hao bado wako.

Utafiti wa mwisho kwenye misitu hiyo ulifanywa mwaka 2004 na kuonyesha kuwa idadi ya nguruwe hao ilikuwa ikididimia zaidi.

"Tuliogopa kuwa wote au wengi zaid walikuwa wametoweka," aliiambia BBC.

Kati ya maeneo saba ambayo wanasayansi waliyafanyia uchunguzi wakitumia kamera fiche, ni matatu tu yaligunduliwa kuwa na nguruwe hao.
Chanzo- BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post