Tuesday, December 19, 2017

ROSE MUHANDO AJIUNGA CCM..,AACHIA WIMBO MAALUM MAGUFULI TUBEBE,USIKILIZE HAPA

  Malunde       Tuesday, December 19, 2017

Msanii wa nyimbo za Injili aliyetamba kwa vibao vyake murua na vyenye kuburudisha Rose Muhando, ametangaza kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi.


Msanii huyo ambaye aliomba kujiunga na chama hicho amekabidhiwa kadi ya Chama cha Mapinduzi jana yeye pamoja na kikundi chake, katika Mkutano Mkuu Maalum wa Tisa wa CCM Taifa, unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, mjini Dodoma.

Rose Muhando kabla ya kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM alitumbuiza kwa kibao maalumu alichokiandaa kwa ajili ya Rais John Pombe Magufuli ambacho amekipa jina la “Magufuli Tubebe”.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey polepole alitangaza kuwa Rose Muhando pamoja na Kundi lake wameomba kupewa nafasi ya kutumbuiza kwa wimbo huo maalumu pamoja na kukabidhiwa kadi za CCM.

“Kundi la Ndugu Rose Muhando na yeye mwenyewe niwakaribishe Jukwani kwa wimbo ambao wameutunga maalumu kwa Ndugu Magufuli. Kundi hili walipokuwa wanakuja walikuwa na maombi mawili, ombi la kwanza ni kupewa nafasi ya kuimba wimbo huu maalumu na pili kujiunga rasmi na CCM,” amesema katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole.

Hata hivyo Polepole amesema kuwa Rose Muhando na kundi lake watakabidhiwa kwa makatibu wa mikoa husika kwa ajili ya michakato ya kuwaandikisha kama wanachama wapya wa CCM.

SIKILIZA WIMBO MPYA WA ROSE MUHANDO MAGUFULI TUBEBE

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post