VIONGOZI WA ACT WAZALENDO WATINGA MAHAKAMANI

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Doroth Semu amefika katika kitengo cha uhalifu wa makosa ya kifedha kilichopo Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Semu amefuatana na Katibu wa Kamati ya Ulinzi ya chama hicho, Mohamed Babu.


Viongozi hao pamoja na Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Yeremia Maganja wanatakiwa kufika katika kitengo hicho wakiwakilisha wajumbe wote wa Kamati Kuu ambao walitakiwa kuripoti leo.

Novemba 2, 2017, Chama hicho kilidai kimepokea wito toka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) wa kuwataka Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya ACT Wazalendo wafike Kituo cha Makosa ya Fedha (Financial Crime Unit) kilichopo Maeneo ya Kamata, Kariakoo Jijini Dar es salaaam kwa ajili ya mahojiano siku ya leo Jumatatu, Novemba 6, 2017. 

Awali, chama hicho kiligoma kuitikia wito huo kwa madai kwamba Jeshi la Polisi halina madaraka ya kushughulikia wala kuingilia maamuzi halali ya vyombo (organs) katika vyama vya siasa na kikasema kuwa kitaendelea na kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani kama kawaida huku kikiwataka Polisi watafute namna na wakati sahihi wa kufanya mahojiano na viongozi wa chama hicho.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.