VIGOGO WA ACACIA WAJIUZULU



Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon
***
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon na ofisa mkuu wa fedha Andrew Wray wamejiuzulu, kampuni hiyo ya uchimbaji wa madini imetangaza.

Kampuni hiyo yenye migodi mitatu ya dhahabu kaskazini magharibi mwa Tanzania imetangaza kuwa wawili hao wataondoka rasmi Acacia mwishoni mwa mwaka huu. Hata hivyo, taarifa inayopatikana kwenye tovuti ya kampuni imeeleza kuwa, Peter Geleta ataiongoza kampuni hiyo katika kipindi cha mpito huku Jaco Maritz akiongoza kitengo cha fedha.

Wateule hao wataanza kazi kuanzia Januari 1, mwaka kesho. Akizungumzia kujiuzulu kwa Brad na Andrew, mwenyekiti wa Acacia, Kelvin Dushnisky amenukuliwa na taarifa hiyo akisema, “Brad na Andrew wamekuwa kiungo muhimu katika uendeshaji na masuala ya fedha hapa Acacia kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne. Kwa niaba ya bodi, ninapenda kuwashukuru kwa mchango wao kwenye kampuni. Tunawatakia kila la heri kwa siku za usoni.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527