TATU MZUKA YAMPONGEZA BI. BUJINGINYA KUTOKA NGARA KWA KUSHINDA MILIONI 50


Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi Bi. Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera alieibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika mwishoni mwa wiki
Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi, Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.
Pichani kulia ni Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera akizungumza jana jijini Dar mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyoibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika mwishoni mwa wiki.Pichani kati ni  mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akiwa pamoja na  Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.
Pichani kati ni mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akiwatambulisha Washindi wa mchezo huo,mbele ya Waandishi wa habari  jijini Dar es salaam.
Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera
ameibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika Jumapili.
***
Bi Bujinginya, mama wa watoto wawili ambaye anaungana na
washindi milioni 130 wa Tatumzuka amesafirishwa kwa ndege kutoka Ngara kuja Dar es Salaam ili kuchukua pesa yake ya ushindi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika juzi Mikocheni.

Baada ya kushinda mara chache katika droo ya kila saa, alipata msukumo wa kuendelea kucheza bila kukata
tamaa.

 "Baada ya kuishi kwa kutafuta pesa ya mlo kila
mwezi na miezi mingine bila pesa, Kiukweli sikujua itakavyokuwa ikifika Januari. Nimefurahi sana kwamba sasa naweza kutembea kwa kujiamini tena baada ya ushindi
huu’ alikiri Bi Bujinginya.

Pia katika tukio la kukabidhi zawadi kwa mshindi
alikuwepo Bwana Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.Dhamira ya Tatu Mzuka ya kubadilisha maisha ya watu haijabadilika
ambapo zimebaki siku chache ili ichezeshwe droo kubwa ya Supa Mzuka jackpot ya milioni 150 jumapili ijayo. Tarehe 19 Novemba saa 3:30 usiku Mtanzania mmoja
ataondoka na kitita cha milioni 150.

"Kila mtu ambaye umecheza tangu Tatumzuka izinduliwe
na kutumia kuanzia shilingi 500 tu kupitia MPESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY, umeingia katika droo hii ambapo unaweza kujishindia milioni 150," alielezea mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba.

Bi Mutahaba aliwahimiza watanzania kuendelea kucheza, akisisitiza kwamba bado washiriki hawajachelewa kujiwekea nafasi ya ushindi huo wa kihistoria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527