MBOWE : MASHA HAKUWA NA MSAADA WOWOTE CHADEMA,ULISHAWAHI KUMSIKIA AMEFANYA CHOCHOTE?

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.


Amesema kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi kuimarika na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.


“Alikuwa hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema Mbowe


Masha alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527