Angalia Picha : KIKAO CHA BODI YA USHAURI YA MKOA WA SHINYANGA KUHUSU UIMARISHAJI WA SEKTA YA AFYAMeneja wa Mradi wa Tuimarishe Afya - HPSS,Manfred Stoemer akizungumza katika kikao nne cha bodi ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga kuhusu Uimarishaji mifumo ya sekta ya afya chini ya ufadhili wa shirika la maendeleo na ushirikiano (SDC) la Uswizi leo Novemba 14,2017 - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

***
Kaimu Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Alfred Shayo amefungua kikao nne cha bodi ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga kuhusu Uimarishaji mifumo ya sekta ya afya chini ya ufadhili wa shirika la Maendeleo na Ushirikiano  la Uswizi (SDC). 

Uimarishaji wa mifumo ya sekta ya afya unatekelezwa na serikali ya mkoa na halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga na mradi wa Health Promotion and System Strengthening (Tuimarishe Afya) HPSS. 

Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Jumanne Novemba 14,2017 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Bw. Shayo alisema mfuko wa bima ya afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) unatekelezwa kupitia mradi wa HPSS kwenye halmashauri za wilaya katika mikoa mitatu pekee nchini ambayo ni Shinyanga,Morogoro na Dodoma. 

Alisema mfuko wa CHF iliyoboreshwa utawanufaisha wananchi endapo elimu zaidi itatolewa kuhusu faida za kujiunga na mfuko huo. 

“Wananchi wanatakiwa kupewa elimu kuhusu mfuko huu,na bahati nzuri mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa mitatu nchini ambayo inafanyiwa majaribio na tunaamini mkoa wetu utakuwa mfano kwa mikoa mingine ambako mfuko wa CHF Iliyoboreshwa utatambulishwa”,alieleza Shayo. 

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume aliwataka maafisa waandikishaji katika mfuko huo kuwa waadilifu kwa kuepuka vitendo vya ubadhirifu wa fedha za mfuko kwani baadhi yao hawafikishi kwenye vituo kwa ajili ya kununua dawa zinaishia kwenye mifuko yao. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Michael Matomora aliwataka wananchi kuondokana na dhana ya kuwa hakuna dawa kwenye vituo vya afya na kuongeza kuwa hivi dawa zote muhimu zinapatikana huku akisisitiza kuwa wananchi wenye kadi za CHF iliyoboreshwa watapewa kipaumbele katika huduma.

Meneja wa Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS), Manfred Stoemer alisema mradi wa HPSS upo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini huku akiwataka wataalamu wa afya kutumia ujuzi na uzoefu walionao katika kuboresha huduma za afya katika vituo.

Aidha wajumbe wa kikao hicho walikubalina kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa CHF iliyoboreshwa huku wakizitaka halmashauri za wilaya kuhakikisha zinasimamia suala la upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KIKAO 
Kaimu Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Alfred Shayo akifungua kikao nne cha bodi ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga kuhusu Uimarishaji mifumo ya sekta ya afya chini ya ufadhili wa shirika la maendeleo na ushirikiano  la Uswizi (SDC) katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Kaimu Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Alfred Shayo akifungua kikao hicho.Kushoto ni Meneja wa Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS),Manfred Stoemer.Kulia ni Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Dkt. Rashid Mfaume. 
Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga,Dkt. Harun Kasale,akifuatiwa na Kiongozi wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga,Profesa Manoris Meshack na Meneja wa Mradi wa Tuimarishe Afya ,Manfred Stoemer. 
Kaimu Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Alfred Shayo akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho 
Wakuu wa wilaya wakiwa ukumbini. Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 
Meneja wa Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS), Manfred Stoemer akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa shughuli za mradi wa Tuimarishe afya.
Mkuu wa Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS),Manfred Stoemer akielezea kuhusu mradi wa Tuimarishe afya. 
Meneja wa Mradi wa HPSS ,Manfred Stoemer akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada kwenye kikao 
Kiongozi wa mradi wa Tuimarishe Afya Tanzania, Profesa Manoris Meshack akizungumza wakati wa kikao hicho 
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati wa kikao hicho 
Meza kuu wakimsikiliza mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rashid Mfaume. 
Meneja wa Mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga, Dkt. Harun Kasale akizungumza katika kikao hicho 
Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lydia Kwezigabo akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa mradi wa HPSS mkoa wa Shinyanga.Alisema hadi kufikia mwezi Oktoba 2017,jumla ya wananchi 37,126 wamejiunga katika mfuko wa CHF iliyoboreshwa. 
Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini 
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniface Butondo (kushoto) na Mwenyekiti wa halmashauri ya Shinyanga,Ngassa Mboje (kulia) wakiteta jambo wakati wa kikao hicho 
Kikao kinaendelea 
Mshauri Mtaalamu masuala ya menejimenti ya dawa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Fiona Chilunda akizungumza ukumbini 
Mshauri Mtaalam masuala ya menejimenti ya dawa Mradi wa Tuimarishe Afya,Fiona Chilunda akisisitiza jambo kwenye kikao hicho. 
Mfamasia wa mkoa wa Shinyanga,John Mfutakamba akichangia hoja wakati wa kikao hicho 
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akichangia hoja wakati wa uwasilishaji mada katika kikao hicho 
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Michael Matomora akichangia hoja ukumbini 
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akizungumza ukumbini 
Afisa ufuatiliaji,tafiti na tathmini mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS),Vicky-Sidney Msamba akichangia hoja wakati wa kikao hicho 
Meneja wa NHIF mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Amani akichangia hoja ukumbini
Mjumbe wa kikao akichangia hoja ukumbini
Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini
Wajumbe wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Wafanyakazi kwenye mradi wa HPSS mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyakazi kwenye mradi wa HPSS wakiwa ukumbini

Mwenyekiti wa kikao nne cha bodi ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga kuhusu Uimarishaji mifumo ya sekta ya afya,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akifunga kikao hicho.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Theme images by rion819. Powered by Blogger.