MTUMBWI WAUA WATU WATATU ZIWA VICTORIA

Watu watatu wamekufa maji ndani ya Ziwa Victoria katika Kisiwa cha Ilamba wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya mtumbwi kuzama.

Watu hao walikuwa wakitoka kuchota maji Kisiwa cha Mazinga. Mwili mmoja umeshaopolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema watu hao walizama jana Jumatatu saa 6:30 mchana.

Amesema miili ambayo haijapatikana ni ya Superius Severine (27) mkazi wa Kijiji cha Nyakitaba na Evelius Zephrine (22) wa Mubunda Kitoko wilayani Muleba

Kamanda Olomi amesema mwili uliopatikana ni wa Adela Andrea (26), mkazi wa Kijiji cha Itongo.

Amesema Nelson Boniphace (20), mkazi wa Kisiwa cha Ilamba aliogelea na kuokolewa.

Mtumbwi huo uliokuwa na madumu 33 ya maji amesema unamilikiwa na Rashidi Sabini (33), mkazi wa Kijiji cha Ilamba.

Amesema mtumbwi huo kutokana na upepo ulipigwa na wimbi hivyo ulipinduka na kuzama.

Via>>Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments