ANGALIA PICHA 13- MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI

Hapa ni katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambapo jana mkuu wa mkoa wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga alikutana na waandishi wa habari kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu ya CCM ya mwaka 2010 kwa kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka 2014

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema katika sekta ya afya serikali imetumia kiasi cha Tsh 4,052,442,249.70 katika kuajiri watumishi wa kada mbalimbali,kukarabati vituo vya afya,ujenzi wa nyumba za watumishi wa sekta ya afya,ununuzi wa vifaa tiba,ujenzi wa zahanati,ununuzi wa gari za wagonjwa,usafirishaji wa wagonjwa kutoka kwenye zahanati mbalimbali na vituo vya afya kwenda kwenye hospitali za wilaya,mkoa na rufaa,ujenzi wa majengo ya zahanati za wagonjwa wa nje(OPD) na kufanya matengenezo ya magari yanayotumika kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa huduma za afya.
Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba 2014 mauaji ya albino yamepungua kwa asilimia 96 na kwamba hali ya ulinzi na usalama mkoani Shinyanga inaridhisha kwa kuwa matukio makubwa ya uhalifu yamepungua sana ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa kuishia mwaka 2010.
 Mkuu huyo wa mkoa alisema  mtandao wa barabara katika mkoa wa Shinyanga una jumla ya kilomita 4862.5
 
 Mkutano huo wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga na waandishi wa habari pia ilihudhuriwa na viongozi wa mkoa wa Shinyanga/wakuu wa vitengo mbalimbali,wa kwanza kulia ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe
 Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi wa mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri


 Katika mkutano huo Rufunga alisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kupeleka watoto wao shule kwa wakati kinyume na hapo serikali itawachukulia sheria

Katika taarifa yake Rufunga alisema katika mwaka 2014 jumla ya shilingi 8,645,146,895.10 zilitumika katika kuboresha sekta ya maji kwa kipindi cha Januari hadi Desemba
 Katika hatua nyingine alisema tofauti na miaka mingine mwaka jana mkoa wa Shinyanga ulijitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya tani 466,979.1 za nafaka,mahitaji ya chakula katika mwaka 2014 yalikuwa tani 380,185.4 na mavuno yalikuwa tani 847,164.5
Aidha alisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kulima zao la mtama hasa katika wilaya ya Kishapu na wilaya ya Shinyanga huku akiwataka wananchi kutunza chakula walichonacho ili kuepuka janga la njaa

Mkuu huyo wa mkoa pia aliyataja baadhi ya maeneo yanayolalamikiwa sana kwa rushwa katika mkoa wa Shinyanga kuwa ni Jeshi la polisi,mahakama ya Mwanzo nguzo nane,Kizumbi na Maganzo na kwa upande wa ngazi za halmashauri ni upande wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya kiwango.

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527