Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Za Chini ya Kapeti!! MH EDWARD LOWASSA AMELAZWA

 
Mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa yako nchini Ujerumani kwa matibabu, imefahamika.

Lowassa ambae wakati wote wa kikao cha bunge hasa kipindi cha majadiliano ya taarifa ya PAC hakuwepo Bungeni, amekuwa Ujerumani ambako amefanyiwa upasuaji wa Kongosho. 

Taarifa kutoka ndani ya familia zinadai kuwa hali ya Lowassa si mbaya sana lakini pia bado haijaimarika. 

Haijaweza kufahamika mara moja kama upasuaji huo ulifanikiwa kumaliza tatizo au la. 

Taarifa za kuugua kwa Lowassa zimefanywa siri kubwa ili kutowakatisha tamaa wafuasi wanaomuunga mkono katika mbio zake za urais 2015.

chanzo-http://mtaaniitz.blogspot.com/

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com