Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ULIZIONA PICHA ZA BASI LILILOACHA NJIA NA KUTUMBUKIA KORONGONI MLIMA KITONGA? ZIKO HAPA

 Basi liitwalo Easy Bus lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa likitokea Lilongwe Malawi likiwa katika mtaro wa Mlima Kitonga.
Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba njia. 
Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga mapema leo baada ya kutumbukia. Hali hii imesababisha foleni kubwa kwa magari huku mengine yakishindwa kuendelea na safari zake.
 Kwa  mujibu wa mashuhuda, chanzo cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote  wakashuka ili kusubiri marekebisho hayo.

Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi, likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.Credit Dj Sek Blog
 Habari za Mapenzi,Simulizi za Mapenzi na Visa vya Mapenzi utazipata Kwa Kubofya Hapa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com