Imeelezwa kuwa mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kupunguza maambukizi ya Ukimwi kwa kufikia kiwango cha 5.1% sawa na asilimia 0.89 ukilinganisha na takwimu ya mwaka jana ambapo maambukizi yalikuwa ni 5.9% huku halmashauri ya Ushetu ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ambayo 6.6%.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba mosi mwaka huu, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ali Nassoro Rufunga alisema takwimu hiyo ni kwa kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, ambapo lengo ni kufanikisha malengo ya taifa ya kufikia sifuri tatu, (maambukizi mapya ya Ukimwi, Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Unyanyapaa) ifikapo mwaka 2025
Alisema Hali hiyo imetokana na viongozi kuendelea kuwaelimisha wananchi kujitokeza kwa hiali kupima afya zao pamoja na kupewa ushauri wa kujikinga na maambukizi pamoja na kutoa ushauri kwa wale wanaogundulika wameambukizwa na kwamba mkoa wa shinyanga utaendelea kutoa elimu hiyo kwa wananchi wote.
Akitoa takwimu ya Maambukizi ya Ukimwi kwa mkoa wa Shinyanga amesema, Halmashauri ya Ushetu inaoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ambayo yanafikia 6.6% Shinyanga 5.9%, Kahama mji 5.2. Kishapu 4.9, Msalala 4.8 na Manispaa ya Shinyana 2.7%
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala amapo maadhimisho ya Siku ya Ukimwi yalifanyika Zabron Donge katika taarifa yake alisema maeneo yanayoongoza kwa kuwa na maambukizi ya Ukimwi ni Maeneo ya machimbo kutokana na mwingiliano wa watu.
Alisema, Kijiji cha Kalole Kata ya Lunguya ambapo kuna wachimbaji wadogo kuna idadi kubwa ya maambukizi ya ukimwi ambapo katika kampeni ya upimaji iliyofanyika hivi karibuni watu 485 walipima ambapo watu 32 waligundulika kuwa na maambukizi sawa na asilimia 6.6.
Aidha aliyapongeza mashirika yasiyokuwa ya kiserikali likiwemo Shirika la Intrahearth, Kiwohede, Huheso Foundation na asasi za dini kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya ukimwi pamoja na kuwawezesha kiujasiliamali watu wanaoishi mazingira hatarishi.
Na Ndalike Sonda-Kahama

Social Plugin