Wanasayansi wakifuatilia kifaa chenye muundo wa kufikiri kama binadamu
Profesa Stephen HawkingProfesa Stephen Hawking
Profesa Stephen Hawking, mmoja wa
wanasayansi mahiri nchini Uingereza, amesema juhudi za kutengeneza
mashine inayofikiria inatishia uwepo wa binadamu.
Anasema :"Kutengenezwa kwa mashine yenye uwezo wa kufikiria inaashiria maangamizi ya binadamu."
Onyo
la Profesa Hawking limekuja kutokana na kuimarishwa kwa teknolojia
anayotumia katika mawasiliano, ambayo inahusisha msingi wa Akili
Bandia(Artificial Intelligence, AI).
Lakini wengine hawana upinzani sana na matarajio ya teknolojia hiyo ya AI.
Mwanasayansi
huyo wa nadharia ya fizikia, ambaye anaumwa ugonjwa wa mishipa ya
fahamu (ALS), anatumia mfumo mpya uliotengenezwa na kampuni ya Intel
kuzungumza.
Wataalam wa mashine za
kujifunza kutoka kampuni ya Uingereza ya Swiftkey pia walihusika katika
kunda mashine hiyo.
Teknolojia yao, tayari inatumika kama mfumo wa
smartphone, unajifunza namna profesa Hawking anavyofikiria na
kupendekeza maneno ambayo huenda angetaka kuyatumia baadaye.
Profesa
Hawking amesema miundo duni ya akili bandia (AI) ambayo imeboreshwa
mpaka sasa imethibitisha kuwa na manufaa sana, lakini ana wasiwasi wa
madhara yanayotokana na kuunda kitu chenye uwezo sawa na binadamu au
kupita. "Mashine hiyo inaweza kujiwasha na kujizima na kujibadili
yenyewe katika kiwango kisichomithilika," amesema.
Cleverbot ni
kifaa(software) ambacho kimeundwa kuwasiliana kama binadamu anavyofanya
"binadamu ambao wana ukomo wa kufikiri kutokana na mabadiliko ya
taratibu ya kibaolojia, hawawezi kushindana na mashine hii, na watapitwa
kwa mbali."
via>>BBC
Profesa Stephen Hawking
Profesa Stephen Hawking
Social Plugin