Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hot News!! MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA KATIBU WA CCM ALIYEUAWA KINYAMA KWA KUCHINJWA HUKO KAHAMA


Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>
Awali waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu nyumbani kwake katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilayani Kahama ambapo mamia ya watu walijitokeza katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa siasa na serikali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja-picha na Mohab Dominic-Kahama
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiaga mwili wa marehemu jana Jumapili katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga-picha na Mohab Dominic-Kahama
Sanduku lililobeba mwili wa marehemu kabla ya mazishi-picha na Mohab Dominic-Kahama

Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Maganga Sengerema akitoa heshima za mwisho kwa marehemu  Daudi Lusalula Mbatiro(56) aliyekuwa katibu  wa CCM kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga aliyeuawa juzi kwa kuchinjwa na watu wasiofahamika eneo la Malenge lililoko kati ya kata ya Kagongwa na Mwalugulu-picha na Mohab Dominic-Kahama
Wa pili kutoka kushoto ni katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Maganga Sengerema akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa Khamis Mgeja(kulia kwake) wakiweka udongo kaburini-picha na Mohab Dominic-Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya  akizungumza baada ya mazishi ambapo alisema serikali  na kamati ya ulinzi imejipanga vizuri kufuatilia tukio hilo na kuomba wananchi kuwa wavumilivu kwani kifo cha Daudi ni pigo kubwa kwa jamii na familia na CCM kwa kupoteza kiongozi wao-picha na Mohab Dominic-Kahama

BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KUHUSU HABARI YA MAUAJI YA KATIBU HUYO WA CCM HUKO KAHAMA

Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com