Kampuni ya ACACIA kupitia mgodi wake wa Buzwagi unatarajia kuanza kuweka taa za barabarani pamoja na Taa za kuongozea magari katika barabara zote za Lami ambazo mgodi huo imejenga pamoja na maeneo mengine muhimu katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa
kutambulisha jina ACACIA, meneja wa
mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Filbert Rweyemamu, alisema ujenzi huo utatekelezwa
ndani ya Miaka miwili ambapo hali hiyo
itasaidia mji wa kahama kuwa na madhali
nzuri nyakati za usiku.
Aidha alisema wao
kama sehemu ya jamii
watahakikisha mji wa kahama wanaweka taa za kuongoza magari (Traffic Lights)
kutokana na mji huo kuwa na ongezeko
kubwa la msongamano wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu, na kwamba
wataendelea kusaidia katika shughuli zingine za maendeleo.
Rweyemamu alipongeza
serikali ya wilaya ya Kahama, kwa kukubali barabara mojawapo iitwe jina la Kampuni (ACACIA ROAD)
ambapo barabara hiyo zamani ilijulikana kama Zongomela Road, hivyo ni faraja
kwao kama wahisani wakuu wa barabara hizo za lami zenye urefu wa kilomita 5.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema Kufanikishwa kwa taa za barabarani na
zile za Kuongozea magari itakuwa faraja kubwa kwa wakazi wa mji huo kwani
watanufaika kwa kuppunguza msongamano na ajali zisizo za lazima.
Alisema Mji wa Kahama utakuwa wa kwanza kupatiwa taa
za kuongozea magari hapa nchini kutokana
na taa hizo mara nyingi kuwekwa katika miji mikubwa pekee hivyo waqnanchi
hawana budi kuendelea kuwaunga mkono wahisani hao
“Ndugu wananchi nipende
kuwapongeza ACACIA Kwa kukubaliana na ombi langu la kuweka taa katika barabara
zote za lami, sasa taa za trafiki zinawekwa na ACACIA, hii itakuwa historia mji
wa kahama kuwa na taa za Kuongoza magari hapa nchini , Tuzidi kuwaunga mkono
watuasidie kupiti mfuko wao wa maendeleo.”alisema Mpesya.
Katika utambulisho huo wa
Jina la ACACIA ambapo awali ilijulikama Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu
African Gold- ABG, uongozi wa ACACIA ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Blad Gordon ulitembelea
baadhi ya Miradi ikiwemo kutembelea barabara za lami mjini Kahama na kituo cha
afya kilichopo kata ya Mwendakulima
ambapo mgodi wa Buzwagi ulipo na kupanda
miti aina ya ACACIA (Kiswahili Mgunga).
BOFYA HAPA TUKUCHEKESHE LEO
BOFYA HAPA TUKUCHEKESHE LEO
Social Plugin