Mama wa kijana anayeugua kifafa
amekataa kumpa mwanawe wa kiume bangi kama matibabu
inavyotakikana-kupitia moshi na mvuke. Mtoto huyo anapasawa kutumia
Bangi kama dawa kupambana na ugonjwa wake wa Kifafa kwa maagizo ya
daktari.
Liam McKnight mwenye umri wa miaka sita napenda kucheza
na ndiye wa kwanza kila mara kukimbia kuelekea mlangoni.Mamake
mzazi,Mandy,anasema kuwa mwanawe anapenda kujua nani anawatembelea.
Familia
hiyo ya McKnight inayoishi jijini Otawa nchini Canada ina wageni wengi
wanaowatembelea-kutoka kwa wanachama wa kukindi cha densi anachoshiriki
binti yao,na hata wauguzi wa kutamka,wa kunyosha viungo vya
mwili,wataalam wa kusikiza-wote wanaomtembelea Liam.
Liam ana
ugonjwa unaojulikana kama Dravet ambayo,ni aina kali sana ya kifafa.Afya
yake hudhoofika mara kwa mara lakini baada ya kufanyiwa majaribio kadha
wa kdha ya matibabu ya ugonjwa huo, anglau hali yake imeimarika kidogo.
Mamake Liam humpa mafuta ya Bangi, ambayo yemtolewa kwa sehemu changa sana ya mmea huo.
Mwezi
Juni mwaka huu,siku kabla Liam kuanza kutumia mafuta hjayo ya
Bangi,(iliyotengezwa kutoka kwa aina ya bangi yenye ufanisi) alizirai
kama mara 67. Katika siku kumi zilizofuatia alizirai tu mara moja.
Tatizo ni kuwa matibabu ya Liam
ni haramu. Kutumia dawa inayotengezwa kwa Bangi inakubalika Canada
lakini lazima iwe tu majani ya Bnagi yaliyokaushwa au mvuke wa majani
hayo.
Kwa Mandy hilo haliwezakni kwa mwanawe kuvuta moshi wa Bangi akiwa umri huo mdogo.
Matoto mdogo anawezaje kuvuta Bangi? anauliza mamake Liam.
Mapema
mwaka 2001, Canada iliruhusu wagonjwa wanaohisi uchungu mwingi kutumia
Bangi kama matibabu. Lakini hakuna majaribio yaliyofanyiwa mafuta ya
Bangi kujua usalama wake kwa afya ya mtu.
Liam ana umri mdogo sana
lakini anaweza kutumia mvuke wa Bangi lakini mamake Liam anasema vipimo
vinyovyofa akwa afya ya Liam ni vya mafuta ya Bnagi.
Mamake Liam
aliwahi kuiandikia serikali Barua kuielezea kuhusu masaibu yake
kuhusiana na matibabu ya Liam. Lakini waziri wa afya alimjibu kwa kusema
anaelewa masaibu ya mtoto Liam wakati akikabiliana na ugonjwa wake
hatari wa kifafa. Lakini alisisitiza kuwa hadi leo serikali bado
haijaidhinisha matumizi ya mafuta ya Bangi wala uuzaji wa mafuta hayo
nchini Canada.
Matumizi ya mafuta ya Bangi, yaliruhusiwa mjini
Minnesota Marekanimwezi Mei, lakini sheria hiyo haitaanza kutumika hadi
Julai mwaka 2015.
Sheria za Bangi kote duniani zinatofautiana.
Mamake
Liam anafahamu kuwa anavunja sheria pamoja na kufahamu athari z
akutumia mafuta ya Bangi. ''Je nahofia kuwa navunja sheria? ndio. Lakini
nahofia zaidi ikiwa hatutafanya chochote hali ya afuya ya mtoto wangu
itazorota.
Kwetu Mafuta ya Bangi ndio tiba anayohitaji mwanangu.
Hatukuwa na mda wa kusubiri majaribio kufanywa. Kwa kila siku, Liam hula
kijiko kimoja cha Bangi ikiwa imechanganywa na mafuta ya nazi.
Social Plugin