Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking News!! MAJAMBAZI YAVAMIA TINDE YAPORA MAMILIONI YA FEDHA


Habari za hivi punde zilizokifikia chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba mji wa Tinde ulioko wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga umevamiwa na majambazi waliokuwa na bunduki usiku huu.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema majambazi watatu waliokuwa na bunduki wamevamia duka la bidhaa mbalimbali la mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Hussein na  inadaiwa majambazi hao wamefanikiwa kuondoka na zaidi ya shilingi milioni 9.

Malunde1 blog imeelezwa kuwa majambazi hao wamevamia duka hilo leo saa mbili usiku,na kwamba baada ya kufika katika duka hilo lililoko katika stendi ya Tinde walikuta wateja na kuwaamuru kulala chini kisha kutekeleza adhma yao.

Habari zinasema kuwa askari polisi wa kituo cha Tinde  kilichopo mita chache kutoka eneo la stendi kulikotokea tukio hilo walifika eneo la tukio baada ya majambazi hao kuondoka eneo la tukio.

Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>  Pia waweza kuwasiliana na Malunde kwa simu/Whatsapp +255 688 405 951 Kama una habari ,picha au Tangazo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com