ANGALIA PICHA- TANESCO YATOA MISAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI KITUO CHA BUHANGIJA _SHINYANGA
Friday, December 05, 2014
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia cha Buhangija mjini Shinyanga. Pichani ni watoto wenye ulemavu wa ngozi wakiangalia zawadi za chakula walizopewa na shirika la umeme Tanesco kanda ya ziwa baada ya kutembelea kituoni hapo ambapo walitoa sukari kilo 50, Mchele kilo 250, Maharage kilo 100, mafuta ya kula ndoo 4, sabuni pamoja na vyandarua 64, huku wakilipia madeni yote ya umeme yaliyokuwa yakidaiwa katika kituo kituo hicho-picha na Marco Maduhu-Shinyanga
Katikati ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Shinyanga Gamba Maugira akikabidhi boksi la sabuni kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino) katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga-picha na Marco Maduhu-Shinyanga
Kushoto ni Meneja mwandamizi wa Shirika la umeme Tanesco kanda ya ziwa Joyce Ngayoma akiwa na meneja wa Tanesco mkoani Shinyanga Gamba Maugira wakikabidhi msaada wa Chakula kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa katika kituo cha buhanghija mjini Shinyanga-picha na Marco Maduhu-Shinyanga
Meneja mwandamizi wa Tanesco kanda ya Ziwa Joyce Ngayoma akikabidhi ndoo ya mafuta ya kupikia kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija-picha na Marco Maduhu-Shinyanga
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin