Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANGANYIKA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika gari maalum mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya ufunguzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika.



Jukwaa kuu ambapo viongozi mbalimbali walikaa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyka.

Maelfu ya wanachi wajitokeza katika maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika leo jijini Dares salaam.
Rais Kikwete akiwa kwenye sherehe hizo.
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara CCM, Philip Mangula. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akisalimiana na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.Baadhi ya viongozi wa nchi wakiwa jukwaa kuu. Askari wa majeshi ya ulinzi na usalama wakitoa heshima kwa Rais Kikwete. Haya ni maonyesho ya halaiki. Baadhi ya wananchi waliofika kwenye sherehe hizo.

RAIS Kikwete leo ameongoza sherehe za kuadhimisha miaka 53 tangu Tanzania Bara ipate uhuru wake Desemba 9 1961. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali nchini na wawakilishi wa nchi za nje walioshuhudia burudani ya kwaya, gwaride, halaiki, ngoma za asili, sarakasi na michezo mingineyo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.


(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com