Mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa mbili katika jiji la Mwanza
leo asubuhi imesababisha athari mbalimbali za kijamii na kiuchumi
yakiwemo mafuriko makubwa, uharibifu wa mali na miundombinu pamoja na
baadhi ya watu kukosa mahali pa kuishi huku familia moja yenye watoto
watano wanaoishi mabatini mtaa wa Mwembegiza wakiokolewa na askari wa
kikosi cha zimamoto na uokoaji baada ya kusombwa na maji.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika maeneo ya mabatini na mwananchi
jijini Mwanza kufuatia mvua kubwa iliyoanza kunyesha majira ya saa moja
asubuhi na kusababisha mafuriko ambayo yalikuwa yakisomba kila kitu,
yakiwemo magari matatu na samani mbalimbali za ndani huku watu wazima 18
ambao walikuwa wamefikia kwenye nyumba za kulala wageni na kwenye
makazi yao halikadhalika wamekijikuta wakiwa hawana la kufanya baada ya
maji kujaa pomoni ndani ya nyumba hizo.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiongea na mtandao huu kuhusiana na
mafuriko hayo, wameishauri serikali kuwaondoa watu waliojenga pembezoni
mwa mkondo wa mto mirongo unaoanzia mto simiyu kufuatia eneo la mabatini
kukumbwa na mafuriko kila mara, huku mmoja wa waathirika wa mafuriko
hayo Nyamhanga Kimore Marwa mkazi wa mabatini mwembegiza akisimulia
mkasa uliomfika wa kupotelewa na watoto wake watano.
Mtandao huu pia umeshuhudia vibao vya alama za barabarani viking’olewa na
mafuriko hayo, magari madogo ya abiria jijini Mwanza maarufu kama
Hiace, yakikwama na kusababisha foleni kubwa kwenye daraja la mwananchi,
baadhi ya magari yaliyokuwa yameegeshwa kwenye gereji jirani na kambi
ya jeshi la polisi yakizingirwa na maji huku pia mapipa ya kuhifadhia
mafuta yakisombwa na mafuriko katika daraja la mtaa wa misheni.
Habari za Mapenzi,Simulizi za Mapenzi na Visa vya Mapenzi utazipata Kwa Kubofya Hapa
Habari za Mapenzi,Simulizi za Mapenzi na Visa vya Mapenzi utazipata Kwa Kubofya Hapa




Social Plugin