KUTANA NA KISIMA CHA MAAJABU,UKINYWA MAJI YAKE UNAFANIKIWA KIMAISHA,KIPO DODOMA,ANGALIA PICHA HAPA

Koo mbili za Wanyazaga na Wambukwa mnyambwa wakiwa wamekusanyika kukizunguka kisima kinachosemekana kimejaa maajabu cha Bwibwi kilichopo Katika kijiji cha Iyumbu kilichopo pembezoni mwa Chuo kikuu cha Dodoma [UDOM] .Unaambiwa ukinywa maji ya kisima hicho unafanikiwa katika maisha yako
Baadhi ya wananchi wakifurahia kutumia maji yanayopatikana kisima cha Bwibwi kilichopo katika kijiji cha iyumbu Manispaa ya Dodoma, kisima hicho kilichovumbuliwa katikati ya miaka 1,800 kiko katika hatihati ya kufukiwa na eneo hilo lituumike kwa matumizi mengine.

Mkuu wa kimila wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akinywa maji yaliyochotwa kisima cha Bwibwi kilichopo Kijiji cha Iyubu Manispaa ya Dodoma, Kisima hicho kinachoaminika ni cha maajabu na mtu anayetumia maji yake hupata Mafanikio ya kiafya na kimaisha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527