TAZAMA PICHA_NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI STEPHEN MASELE ACHANGISHA MILIONI 115 KWA AJILI YA UJENZI WA WODI YA WAZAZI KITUO CHA AFYA KAMBARAGE MJINI SHINYANGA

Hapa ni katika viwanja vya kituo cha afya cha Kambarage mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika harambee kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi(akina mama) katika kituo hicho kinachotumiwa na wakazi wa kata ya Kambarage na maeneo mengiya mji wa Shinyanga na nje ya Shinyanga.Mgeni rasmi alikuwa naibu waziri wa nishati na madini na mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi mheshimiwa Stephen Masele aliyekusanya viongozi wa siasa na serikali,wafanyabiashara,wachimbaji wa madini na wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuchangia harambee hiyo.Lengo lilikuwa ni kupata shilingi milioni 105,lakini zilizopatikana ni milioni 115,ambazo ni zaidi ya 100% zilizotakiwa-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Wa kwanza kulia ni naibu waziri wa nishati na madini na mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi mheshimiwa Stephen Masele,aliyeshikilia kipaza sauti ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Khamis Mgeja akizungumza katika harambee hiyo ambapo aliwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono mbunge wao katika shughuli za maendeleo na kwamba amefurahishwa na kitendo cha mbunge huyo kuwa mstari wa mbele katika harambee ya kujenga wodi kwa ajili ya akina mama huku akipongeza kazi mbalimbali zinazofanywa na wabunge mkoa wote wa Shinyanga na watendaji wa serikali.Pia aliwaasa kuunga mkono shughuli za maendeleo bila kujali itikadi ya kichama kwani watanzania wanahitaji maendeleo-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Pamoja na umuhimu wa harambee hiyo,watu wachache walijitokeza huku wakuu wa wilaya kutoka maeneo mbalimbali nchini wakijitokeza kwa wingi(hawapo pichani) kumuunga mkono mheshimiwa Masele.Viongozi wengi wa Shinyanga hawakuwepo katika harambee hiyo-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

 Waandishi wa habari wakiwa katika eneo la tukio lililohudhuriwa na wakuu wa wilaya mbalimbali nchini,wafanyabiashara,wachimbaji wa madini(wakubwa,kati na wadogo),wenyeviti na wakurugenzi mbalimbali wa halmashauri,viongozi wa siasa(wabunge na madiwani) na serikali,waandishi wa habari na wananchi wenye mapenzi mema-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Aliyeshikilia kipaza sauti ni diwani wa kata ya Kambarage mjini Shinyanga( kilipo kituo cha afya cha Kambarage) kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Nyangaki Shilungushela (Mzee wa Utaratibu)akizungumza wakati wa harambee hiyo ambapo alisema kata yake ina Uzito(wanaiogopa) ndiyo maana Viongozi wa CCM wamefanya harambee hiyo katika kata yake.Wa pili kutoka kulia ni mshereheshaji(MC) katika harambee hiyo ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Easy Flex Production Happness Kihama -Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Harambee inaendelea_Watu walikuwa wachache sana,wengi walikuwa wageni tena kutoka nje ya Shinyanga waliofika hapo kwa nguvu za mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Wakati harambee inaendelea,mvua nayo ikanyesha,wengine walijifunika viti ili wasinyeshewe mvua-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

 Picha ya pamoja mgeni rasmi Stephen Masele(wa 3 kutoka kushoto)na baadhi ya wakuu wa wilaya ,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,waliohudhuria harambee hiyo na kuchangia mamilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi huku wenyeji wakidaiwa kuingia mitini pamoja na kwamba walipewa barua za mialiko

TAZAMA PICHA ZAIDI ZA PAMOJA HAPA CHINI KWA MAKUNDI MBALIMBALI BAADA YA HARAMBEE HIYO

 Picha ya pamoja na mgeni rasmi aliyechangia shilingi milioni 45 katika harambee hiyo huku jumla kuu iliyopatikana ni milioni 115 wakati lengo lilikuwa ni kupata shilingi milioni 105 tu -Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 Picha ya pamoja mganga mkuu wa kituo hicho cha afya Dkt. Costantine Hubi anasema kituo cha afya cha Kambarage kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa jengo la kujifungulia wajawazito,ukosefu wa wodi maalumu ya wajawazito kabla ya kujifungua, wakati wa kujifungua na baada ya kujifunguana ukosefu wa chumba cha upasuaji wa dharura kwa wajawazito wenye uchungu pingamizi sambamba na ukosefu wa  gari la kubeba wagonjwa -Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 Picha ya pamoja-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 Picha ya pamoja-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 Picha ya pamoja-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Picha ya pamoja-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Picha ya pamoja waandishi wa habari na mgeni rasmi

Picha ya pamoja-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527