TAZAMA PICHA MAZISHI YA ALIYEKUWA MHADHIRI MWANDAMIZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM DK KAPOLI,WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AONGOZA MAZISHI


Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa mhadhiri chuo kikuu cha Dar es salaam Dk Kapoli aliyefariki dunia Jumamosi alfajiri wiki iliyopita akipata matibabu katika hospitali ya Tumbi huko Kibaha,alipokimbizwa hospitalini hapo akisumbuliwa na BP na Kisukari.Mazishi yamefanyika Julai 28, 2014,yakiongozwa na waziri mkuu Mizengo Pinda
Dr. Irenius Kapoli enzi za uhai wake
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika mazishi ya Mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dk, Irenius  Kapoli, nyumbani kwa Marehemu, Mbezi Malamba Mawili jijini Dar es Salaam Julai 28, 2014.
 Waomboleaji wakiwa  wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dk, Irenius Joseph Kapoli, katika mazishi  yaliyofanyika nyubani kwa Marehemu,  Mbezi Malamba Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014
 Mwili wa  aliyekuwa Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini,  Dk, Irenius Joseph Kapoli, ukitemswa kaburini katika mazishi  yaliyofanyika  nyumbani kwa Marehemu,  Mbezi Malamba Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014.

Dr Ireneus Kapoli amefariki dunia (Jumamosi)alfajiri katika hospitali ya Tumbi huko Kibaha kutokana na BP na Kisukari. 

 Alikimbizwa hospitalini baada ya kuugua ghafla.  

Dr Kapoli alikuwa mtaalam wa lugha ya Kiingereza na alifanya PHD yake nchini Uingereza ,alianza kufundisha Main Campus Mlimani baadaye kuajiriwa katika Shule Kuu ya Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma(sjmc).


 Alifundisha kwa muda wa zaidi ya miaka 10 hapo UDSM-SJMC,akiwa katika idara ya Lugha na  alistaafu rasmi mwaka jana.

Mbali na kufundisha smjc Dr Kapoli aliwahi kufanya kazi maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kozi alizopata kuzifundisha katika chuo hicho enzi za uhai wake ni "Communications Skills( English for Journalists/Media),"Critical Discourse Analysis" na "Critical Thinking and Argumentation"

Dr Kapoli alikuwa mtanashati,mpenda haki,mshauri mzuri,
mwalimu bora, mwenye msimamo hakupenda upumbavu hata kidogo,,hakika aliyefundishwa na mwalimu huyu atakumbuka mengi mema ya Dr Kapoli.


Hata mkurugenzi wa blog hii ya Malunde1 ndugu Kadama Malunde alifundishwa na Dr Kapoli wakati akiwa mwanafunzi katika chuo hicho mwaka 2008/2011.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Dkt Kapoli.Amina

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527