MWANAMKE AANGUKA CHOONI NA KUPOTEZA MAISHA WAKATI WA SWALA YA IDD HUKO IRINGA

Halida Ng’anguli akiwa ameanguka  nje ya  choo  katika  uwanja  wa Samora kabla ya  kufariki dunia

WAKATI  waislamu   nchini  jana  wameungana na  waislamu  wenzao duniani kuswali  sala  ya Iddi mkoani  Iringa swala   hiyo  imemalizika  vibaya  kufuatia kifo  cha  muumini  mwenzao Halida Ng’anguli mkai  wa Mwangata  C ambae ni shangazi wa manahabari wa gazeti la majira  Iringa Zuhura  zuhkeri kufariki  dunia  baada ya masaa machache  toka aanguke chooni uwanja wa  Samora.

Tukio  la  kuanguka kwa mwanamke   huyo  lilitokea majira ya  saa tatu  asubuhi wakati  waumini  wa dini ya  Kiislamu  ambao  walikuwa  wakiswali pamoja  katika  uwanja  wa samora mjini Iringa  kumaliza swala na  kuanza maandalizi ya kuondoka  uwanjani  hapo kabla ya mmoja kati ya  viongozi  kwa kutumia kipasa  sauti  kutangaza  tukio la  kuanguka kwa mwanamke  huyo huku akiwataka  wanawake kwenda  eneo la tukio katika  vyoo vya wanawake  ili  kutoa msaada  zaidi.

Hata  hivyo  jitihada za  waumini  hao wanawake  pamoja na  askari  waliokuwepo  uwanjani hapo  zilifanikisha  kumkimbiza  mwanamke  huyo  hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi. 

Mbali ya  jitihada  kubwa  za madaktari wa Hospitali  hiyo  kutaka kunusuru maisha  yake  bado  hali ilionekana  kuwa mbaya  zaidi kutoka na tatizo ya  ugonjwa wa kisukari lililokuwa  likimsumbua .

Yapata  majira ya saa 4  usiku mwanamke  huyo alifariki dunia  wakati  akiendelea  kupatiwa matibabu  Hospitalini  hapo.

Akithibitisha   kutokea  kwa  kifo  hicho Shangazi wa marehemu  mwanahabari  Zuhura Zukheri alisema  kuwa shangazi yake  alifariki  majira ya saa 4 akiwa katika matibabu na  kuwa  toka  alipofikishwa  Hospitali hapo  hali yake  ilikuwa  mbaya na  hakuweza kupata nafuu.

Zuhura  alisema  kuwa tatizo kubwa  lililokuwa likimsumbua ni ugonjwa wa  Kisukari  na  kuwa shughuli za mazishi  zimepangwa  kufanyika  leo  ambayo ni  siku ya  Iddi pili majira ya saa 10 jioni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527