Monica Kabati kutoka musoma mmoja wa majeruhi ambaye bado yupo katika moja ya wodi katika hospitali ya mkoa |
Treni ikiwa imehama kwenye njia yake |
Basi la saibaba likiwa limepasuka taili baada ya kuburuzwa umbali wa mita 30 |
Mwandishi wa habari wa ITV na Radio one Stephen Wang'anyi kichukua matukio jana usiku |
Basi la saibaba baada ya kunasuliwa leo asubuhi |
Watu 24 wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea jana usiku
majira ya saa tatu na nusu, ambapo Basi la Saibaba T687 BUW likitokea Dar es
salaam kuelekea mwanza liligonga Treni ya abiria iliyokuwa inatokea Mwanza
kwenda Dar es salaam katika eneola
Kalogo barabara ya kwenda Mwanza mjini shinyanga.
Mganga mfawidhi wa
hospitali ya mkoa wa shinyanga Dk Fredrick Mlekwa ameiambia
malunde1.blogspot.com kuwa hadi sasa kati ya majeruhi 24 waliofikishwa katika
hospitali hiyo ya mkoa majeruhi waliobaki ni 6 na wengine wameruhusiwa jana na leo asubuhi.
Kamanda wa jeshi la
polisi mkoa wa shinya ACP ambaye alikuwepo katika eneo la tukio akiwa na
maafisa wengine kibao was polisi amesema chanzo cha ajali hiyo bado
hakijajulikana na kwamba atatoa taarifa kamili hapo baadae kwani uchunguzi bado
unaendelea.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema ghafla walisikia sauti ya
mpasuko wa taili za gari baadae kuona basi limenasa kwenye treni huku baadae
maafisa wa polisi walifika na majeruhi wakikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa
shinyanga.
Dreva msaidizi wa basi hilo bwana Hussein Mohamed amesema
walipofika eneo la kalogo ghafla walishtukia gari lao limeburuzwa kwa umbali wa
takribani mita 30 kutoka barabarani na kuongeza kuwa treni hiyo haikupiga honi
na haikuwa imewasha taa.