Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

355 WASHIKILIWA MKOANI MWANZA KWA WIZI NA UPORAJI WA OKTOBA 29



Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanya msako na kufanikiwa kuwakamata jumla ya wahalifu wapatao 355 ambao wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo wizi na uporaji walioufanya wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Kulingana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi Wilbroad Mutafungwa, Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimewakamata Jumla ya watu wengine 116 kwa tuhuma za uchochezi na kuhamasisha maandamano haramu wanayopanga kuyafanya Jumanne ya Disemba 09, 2025.

Kulingana na Kamanda Mutafungwa watuhumiwa 355 waliokamatwa walikutwa na Mitungi 118 ya gesi ya Kampuni ya Lake Oil Oryx na Mihan, Magodoro 40 aina ya Super Banco na Tanform pamoja na jora 18 za Vitambaa vya kushonea magodoro.

"Watuhumiwa wengine wamekamatwa na difu 1 ya gari, Injini 3 za magari, Gear boksi, Mashine 2 za ATM, Matenki 4 ya maji, Fire Extinguisher 3, Compresser 01, Pipa 4 za Kemikali za kutengenezea magodoro, Friji 1 aina ya Voni, Kasiki 2, ndoo za rangi pamoja na mabati 14." Amesema Kamanda Mutafungwa.

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kando ya kueleza kuendelea na doria katika Mkoa mzima wa Mwanza, katika taarifa yake kwa umma limetoa rai kwa wananchi kutokubali kushirikishwa kwenye maandamano haramu yaliyopigwa marufuku hapo Disemba 09, 2025, Wazazi na walezi wakitakiwa kuwazuia watoto wao kutojiingiza kwenye maandamano na badala yake washirikiane na serikali kuimarisha amani na utulivu kwenye siku hiyo muhimu ya kumbukizi ya Tanzania kupata uhuru wake.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com