PAPA FRANCIS ATEUA MRITHI WA KADINALI PENGO

Papa Mtakatifu Francis amemteua Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi kurithi Jimbo kuu la Dar es Salaam, Tanzania.

Katika barua iliyotolewa na na Katibu Mkuu TEC, Raymond Saba imesema kwamba Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi alikuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania. 

Kwa uteuzi huo wa Papa Francis, Askofu Ruwaichi atachukua nafasi ya Polycarp Pengo.

Askofu Mkuu Ruwaichi alizaliwa tarehe Januari 30, 1954, huko Mulo, Kilema, Jimbo Katoliki la Moshi na baada ya masomo na mafunzo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre Novemba 25, 1981 na Februari 9 1999, akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Mbulu na kuwekwa wakfu tarehe 16 Mei 1999.

Tarehe 15 Januari 2005, Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua Askofu Ruwaichi kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma na kusimikwa rasmi tarehe 19 Februari 2005

Hata hivyo 2011 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza na kusimikwa rasmi tarehe 9 Januari .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527