HIZI NDIYO TIMU 5 AMBAZO HAZINA UZOEFU KOMBE LA DUNIA 2018

Kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2018 zinazoanza Alhamisi Juni 14 nchini Urusi, yafuatayo ni mataifa ambayo wachezaji wake wamechezea mechi chache zaidi katika timu zao hivyo kuwa na uzoefu mdogo.

Timu ya taifa ya Uingereza imeingia kwenye orodha hiyo ikiwa na kikosi cha wachezaji 23 ambao wameichezea timu hiyo kwa jumla ya mechi 465 hivyo kushika nafasi ya pili katika timu ambazo hazina uzoefu.

Nafasi ya tano inashikiliwa na timu ya taifa ya Serbia ambayo wachezaji wake 23 waliokwenda Urusi wameichezea timu hiyo jumla ya mechi 563. Nafasi ya nne inashikwa na Morocco ambayo wachezaji wake wameicheze mechi 522.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na timu ya taifa ya Senegal ambayo yenyewe nyota wake 23 waliokwenda Urusi wameichezea mara 516 hivyo kuwa ni kati ya nchi ambazo zina uzoefu kidogo.

Orodha hiyo inakamilishwa na timu ya taifa ya Tunisia ambayo yenyewe imekusanya vijana wadogo ambao wameichezea timu hiyo mara 462. Tunisia inakamilisha nchi tatu za Africa ambazo zipo chini kwenye suala la uzoefu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527