RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, John Pombe Joseph Magufuli
amewakabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba
SC wakitoka kufungwa 1-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam Mei 19, 2018.
Kabla
ya kuwakabidhi Kombe hilo, Rais Magufuli akawaambia Simba SC
hajaridhishwa na kiwango cha mchezo wao na akawataka wakakiboreshe
kuelekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Pamoja
na hayo, Rais Magufuli amewapongeza Simb SC kwa kufikia kutwaa la
ubingwa wa Ligi Kuu bila ya kupoteza mechi kabla ya kufungwa na Kagera
leo.
“Mimi
huwa ninafuatilia ligi mbalimbali, nilifuatilia hadi juzi timu ambazo
zilikuwa zimechukua ubingwa bila kufungwa, zilikuwa zimebaki mbili,
Barcelona na Simba, Jumapili iliyopita Barcelona wakafungwa na leo Simba
nao wamefungwa,”alisema Rais Dk. Magufuli kabla ya kuwakabidhi Kombe
hilo Simba SC.
Rais
amesema kwamba anawapongeza Simba SC kwa sababu pia wamepitia kipindi
kirefu bila kuchukua ubingwa na akasema anazipongeza na timu nyingine
zilizoshiriki Ligi Kuu msimu huu huku akiwatania SImba; “Nashukuru
hakuna timu iliyokwenda FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) kudai
pointi za mezani msimu huu,”.
Aidha,
Rais Magufuli aliyewapongeza Kagera Sugar kwa kuonyesha mchezo mzuri
leo pia alisema Simba SC nayo ilijitahidi na kudhihirisha wao ni
mabingwa.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na marefa Florentina Zablon wa Dodoma
aliyesaidiwa na Jesse Erasmo wa Morogoro na Mashaka Mwandile wa Mbeya,
bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba
SC, Edward Christopher Shijja kwa kichwa dakika ya 84 akimalizia krosi
ya Japhet Makalai kutoka upande wa kulia.
Mshambuliaji
Mganda, Emmanuel Okwi akapoteza nafasi ya kuisawazishia Simba SC dakika
ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kukamilika kwa dakika 90 za kawaida
kufuatia mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na kipa Juma Kaseja.
Florentina
Zablon aliwapa Simba penalti hiyo baada ya Okwi mwenyewe kuangushwa na
kiungo mkongwe wa Kagera Sugar, George Kavilla.
Simba
SC inabaki na pointi zake 68 baada ya kucheza mechi 29 na itakwenda
mjini Songea kukamilisha msimu kwa kumenyana na wenyeji Maji Maji Mei 28
Uwanja wa Maji Maji. Kagera Sugar inafikisha pointi 34 katika mechi ya
29, ingawa wanabaki nafasi ya 10.
Kikosi
cha SimbaSC kilikuwa; Said Mohamed Nduda, Nicholas Gyan/Muzamil Yassin
dk46, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Paul Bukaba, James Kotei/Salim
Mbonde dk50/John Bocco dk70, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shomari Kapombe,
Emmanuel Okwi, John Bocco, Shiza Kichuya,